STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 25 Aprili 2015

SIMBA MWENDO MDUNDO WAEDELEA KUIFUKUZIA NAFASI YA PILI KWA UDI NA UVUMBA, WAICHAPA NDANDA FC 3-0 TAIFA




Wekundu wa Msimbazi Simba SC, leo wameendelea kuuhakikishia umma wa mashabiki wake kuwa bado wanasaka nafasi ya pili kwa udi na uvumba baada ya kutoa kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 3-0 dhidi ya Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara, katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba ambao leo walionekana kuwa na ari ya hali ya juu, waliuanza mchezo huo kwa kasi ambapo dakika ya tatu tu ya mchezo, kiungo mahiri wa timu hiyo Said Ndemla aliachia shuti kali na kutoka sentimita chache tu kutoka langoni mwa timu ya Ndanda.
Lakini Ndanda nao walijibu mashambulizi langoni mwa Simba katika dakika ya sita lakini Masoud Ally alipiga shuti ambalo lilitoka nje.
Simba walifungua karamu ya mabao mnamo dakika ya nane ya mchezo kutoka kwa Jonas Mkude, baada ya kuachia shuti kali kutoka nje ya eneo la hatari la Ndanda kutokana na makosa yaliyofanywa na walinzi wa timu hiyo na kutinga moja kwa moja langoni mwa Ndanda.
Simba waliendelea kulisakama lango la Ndanda na kufanikiwa kupata penati manamo dakika ya 11 baada ya Emmanuel Okwi kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari, lakini penati iliyopigwa na Ibrahim Hajib ilipaa juu kabisa mwa lango la Ndanda.
Lakini haikuishia hapo, Simba waliongeza goli la tatu katika dakika ya 15 kupitia kwa Ramdhan Singano 'Messi' kutokana na uzembe uliofanywa na mlinda mlango wa Ndanda baada ya kuutokea mpira na kuukosa.
Katika dakika ya 36, mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Hajib ulitua kichwa mwa Okwi na kutinga nyavuni mwa Ndanda, lakini mwamuzi alikataa bao hilo akidai kabla Okwi kufunga goli hilo alikuwa ameotea.
Ibrahim Hajib, ambaye leo hakuwa kwenye kiwango chake alikosa nafasi nyingine ya wazi dakika ya 40 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Okwi, lakini hata hivyo mpira ambao aliu'chop' ulitoka umbali mdogo kutoka langoni mwa timu ya Ndanda.
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Simba waliokuwa wakiongoza kwa magoli 3-0.
Kipindi cha pili Ndanda walionekana kuzinduka baada ya kuanza kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa Simba na kuafanikiwa kupata goli dakika ya 46 lakini Stamili Mbonde ambaye ndiye alifunga goli, alikuwa tayari ameotea hivyo mwamuzi kulikaa goli hilo.
Simba walifanya shambulizi la hatari langoni mwa Ndanda baada ya mshambuliaji Simon Sserunkuma kupiga krosi nzuri lakini mshambuliaji kinda wa timu hiyo ambaye alitokea benchi alikosa goli hilo.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joseph Owino, Juuko Murusheed, Jonas Mkude, Said Ndemla, Awadh Juma/William Lucian ‘Gallas’ dk76, Ibrahim Hajib/Simon Sserunkuma dk54, Emmanuel Okwi na Ramadhani Singano ‘Messi’/Issa Abdallah dk69.
Ndanda FC; Salehe Malande, Azizi Sibo, Shukuru Chachala/Stahmili Mbonde dk49, Ernest Mwalupani, Cassian Ponera, Zablon Raymond, Jacob Massawe, Hemed Khoja, Gideon Benson/Rajab Isihaka dk70, Masoud Ally/Omar Mponda dk57 na Kiggi Makassy.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox