Kocha
wa Chelsea Jose Mourinho, amekubaliana na kauli ya Nguli wa zamani wa
Arsenal Thiery Henry (TT), kuwa endapo Arsenal itafanya usajili wa
wachezaji wanne wa kiwango cha dunia, basi wanaweza kuirudia rekodi yao
ya mwaka 2004 ambapo walimaliza ligi bila ya kufungwa.
Jumatatu
ya wiki hii, Henry alisema kuwa Wenger anahitaji kuongeza wachezaji
wanne tu wenye ubora wa hali ya juu kabisa ili kuweza kupambana na
Chelsea katika kutafuta taji la ligi kuu msimu ujao.
"Arsenal
wana kikosi cha kutisha sana. Lakini wanahitaji kuongeza wachezaji
wanne tu, wakifanya hivyo nakuhakikishia kuwa watamaliza msimu bila ya
kufungwa tena kama ilivyokuwa msimu wa 2003/2004.
Mourinho
pia kwa upande wake aliongeza kuwa klabu kama Manchester United,
Liverpool na Manchester City nao watafanya usajili wa nguvu katika
dirisha la usajili litakaloanza mwishoni mwa msimu huu kutokana na
matokeo yasiyoridhisha walioyapata msimu huu.
Mourinho:
"Manchester United wana kikosi ambacho ninaweza kusema ni bora kabisa,
ukizingatia wana mchezaji ambaye alivunja rekodi ya usajili ligi kuu
nchini Uingereza, Angel Di Maria, ambaye hata hivyo pia hana nafasi
katika kikosi hicho.
"Hii
inaonesha jinsi gani wana kikosi bora . Ni klabu ambayo ambayo
'Financial Fair' haina nafasi kubwa sana na wanaonekana bado wana nafasi
kubwa sana ya kuboresha kikosi katika dirisha la usaji litakaloanza
mwishoni mwa msimu.
"City
nao wamefanya vizuri sana, kushinda mataji mawili ndani ya miaka mitatu
na bado pia wanaonekana wana ni ya kuboresha kikosi chao mwishoni mwa
msimu pia, sawa sawa kwa upande wa Liverpool.
"Msimu
ujao utakuwa ni mgumu sana kuliko huu unaoelekea mwishoni. Ni ngumu
sana kwa timu kutawala kwa kipindi kirefu. Hapa sio Ujerumani ambapo
Bayern Munich wanatawala. Sio Uswizi ambapo kuna FC Basel. Na wala sio
Scotland ambapo Celtic ndiyo vidume. Ni ngumu sana hapa kwa kweli."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni