YANGA wanakwea pipa leo usiku kuwafuata Etoile du Sahel kucheza mechi ya marudiano ya hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho.
Mechi
ya kwanza jijini Dar es salaam, timu hizo zilitoka sare ya 1-1, hivyo
Yanga wanahitaji ushindi au sare ya kuanzia magoli 2-2 ili kusonga mbele
moja kwa moja.
Mkuu
wa idara ya habari na mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro ameuambia
mtandao huu jioni hii kuwa kikosi cha Yanga kitaondoka na Ndege ya
biashara ya Emirates majira ya saa 4:25 usiku na kitapitia Dubai.
"Vijana
wanaondoka leo usiku saa 4:25 na ndege ya Emirates kupitia Dubai".
Amesema Muro na kusema: "Vijana wana morali, mimi nakwambia lazima jamaa
(Etoile) waloe, unajua hakuna kitu kibaya kama watu dhaifu kujipanga na
kucheza kama siafu, wanakuwa na nguvu kubwa, wao wanajiona wana mpira
mkubwa sana, watacheza kwa kujiamini, sisi tutashambulia"
"Wakikaa
mara mbili tu watalala, uwezekano wa kuondoka na ushindi ni mkubwa
sana. Babu ( kocha Hans van der Pluijm) ana matumaini makubwa sana na
kikosi chake, ana imani ya vijana wake kufanya vizuri".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni