SKY
Sports wamefanya tafiti kuonesha ni timu gani England imefanya vizuri
zaidi katika miaka 50 iliyopita na wametengeza data kwenye jedwali
kuonesha matokeo.
Nafasi
katika jedwali imetolewa kwa kuangalia wastani wa nafasi inayomaliza
timu katika mIsimu yote ndani ya kipindi cha nusu karne.
Ili
kukidhi vigezo vya utafiti huo, timu pekee ambazo zimemaliza nafasi nne
za juu kwenye ligi za England angalau kwa miaka 15 iliyopita tangu
1964-65 zimejumuishwa.
Jumla ya timu 90 zimejumuishwa katika utafiti huo.
Liverpool
imeongoza kwenye wastani wa ligi kuu ambao ni wastani wa 3.3 na sasa
wapo nafasi ya tano katika msimamo msimu huu, lakini hawajahi kushinda
kombe kwa miaka 26 sasa.
Manchester United imeshika nafasi ya pili kwa wastani wa ligi wa 4.9
Arsenal (4.9) wameshika nafasi ya tatu, wakiuatiwa na Everton (8.8), Tottenham (9) na Chelsea (11).
TIMU YA KWANZA MPAKA 20 SOMA CHINI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni