DIDIER
Drogba jana amehudhuria Shoo ya Chelsea Friday night kuzungumzia
furaha yake wakati huu akitarajia kushinda kombe lake la nne la ligi kuu
England kesho jumapili.
Chelsea
wanahitaji pointi tatu tu kujitangazia ubingwa na wanaweza kufanya
hivyo kama watashinda mechi ya kesho dhidi ya Crystal Palace.
Drogba
amesema anajivunia makombe aliyobeba mpaka sasa na baada ya kurudi tena
klabuni kumalizia soka lake, amejawa na furaha ya kuvaa medali nyingine
kwa kutwaa taji la EPL.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni