Kocha
wa Real Madrid Carlo Ancelotti amemkingia kifua Cristiano Ronaldo kwa
vitendo vyake anavyovifanya na kusema kuwa anashangazwa sana na baadhi
ya mashabiki wa klabu hiyo kumpigia miruzi inayoashiria kutofurahishwa
na tabia zake pindi awapo uwanjani.
Ronaldo
alifunga bao la 50 kwa msimu huu katika michuano yote nchini Uhispania,
Aprili 18 dhidi ya Malaga, lakini ameshindwa kuziona nyavu ndani ya
michezo mitatu aliyocheza hivi karibuni.
Ronaldo
alishambuliwa vibaya na mashabiki wa klabu yake baada ya kuonesha
kitendo kisicho cha kiuanamichezo pindi Alvaro Albeloa alipofunga goli
dhidi ya Almeria, ambapo Real walishinda 3-0.
"Nadhani
kama Ronaldo amefunga mabao 50, hiyo ni kwa sababu ya asili yake,"
Ancelloti alisema. "Hafurahishwi na anachokifanya, ndio maana muda wote
huwa anapambana.
"Ndio maana huwa anafunga magoli 50 kwa msimu, na amekuwa akifanya hivyo kwa kipindi kirefu sana.
"Yaani sielewi kwa nini mashabiki wanampigia miruzi Ronaldo."
Ronaldo
alinekana kutofurahishwa na goli la Arbeloa baada ya kuupiga mpira
wavuni kwa hasira na pia kutoenda kujumuika na wenzake katika
kutoshangilia goli hilo, kitendo kilichofsiriwa na wengi kuwa ni cha
ubinafsi kwa mchezaji huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni