BONDIA mahiri wa
Uingereza Amir Khan amesema meneja wa Floyd Mayweather amemwambia kuwa
pambano lao linawezekana baada ya Mmarekani huyo kumtandika Manny
Pacquiao jijini Las Vegas.
Mayweather mwenye umri wa miaka 38
aliendeleza rekodi yake ya kutopigwa katika mapmbano 48 kwa kushinda kwa
alama katika pambano dhidi ya Pacquiao.
Khan mwenye umri wa miaka 28
ambaye atapambana na bingwa wa zamani wa dunia wa uzani mwepesi wa
welter Chris Algieri Mei 30 mwaka huu amesema pia amealikwa kupigana na
Pacquiao mwenye umri wa miaka 36.
Akihojiwa Khan amesema yuko katika
nafasi ya kupambana yeyote kati ya hao wawili lakini yeye anamtaka
Mayweather. Khan aliendelea kudai kuwa meneja wa Mayweather, Len Ellerbe
alimfuata baada ya pambano hilo na kumwambia kuwa kifedha wanajua
litakuwa pambano kubwa hivyo anadhani timu ya Mayweather inahitaji
pambano hilo huku timu ya Pacquiao nayo ikihitaji kitu kama
hicho.
Mayweather amesema baada ya pambano lake kuwa amepanga kustaafu
baada ya pambano kupigana pambano moja zaidi Septemba mwaka huu
kwasababu hafurahii tena mchezo huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni