Kocha wa Arsenal aliachwa amechanganyikiwa asijue la kufanya baada ya nafasi yake ya kumaliza katika nafasi za juu katika ligi kuanza kuingia wasiwasi,Arsenali haijawahi kushika nafasi ya pili wala ya tatu kwa takribani miaka kumi hadi sasa na ushindi wa Swansea pale nyumbani kwao uwanja wa Emirates umeongeza wasiwasi huo.
Arsenal walitawala mechi kipindi cha pili lakini juhudi zao zilikwamishwa na golikipa wao wa zamani Lukas Fabianski baada ya kufanya kazi nzuri na baadae kabisa kazi ilimalizwa na Bafitembi Gomis kwa kichwa na kuihakikishia pointi zote tatu kwa vijana wa Garry Monk,
Japokua wamepoteza mchezo huo lakini kocha wa Arsenal anaamini wataisambaratisha Manchester United jumapili ijayo na kupata ushindi wao wa kwanza katika mechi kumi za ligi walizokutana.
“inachanganya sana kwa sababu tumepoteza mchezo sehemu ambayo hatukutakiwa na kulikua hakuna hatari wala presha yoyote”
“hatukumalizia vizuri,hatukua na utulivu na tulifanya kosa katika eneo la ulinzi.Hatukua na bahati leo.
“lakini kwa ujumla tumepata mazuri kwenye mchezo wa leo na kwa bahati mbaya mechi kama hizi unaweza kucheza 20 nakushinda 19 na kupoteza mmoja.na huo mmoja ndio huu wa leo.
Na alipoulizwa ni mambo gani mazuri ameyapata kutokana na mchezo wa leo alijibu “tumemiliki na tumeonyesha mchezo mzuri sana na mchezo ulikua na ubora wa hali ya juu sasa tunahitaji kurudi na kujiandaa na mchezo unaofuatia”.
“Wachezaji wangu waliniangusha lakini hatutaki haya yatokee tena jumapili,ni mechi muhimu sana”.
Fabianski alikua imara sana na kwa kuzuia michomo kadhaa kutoka kwa Sant Cazorla,Alexis Sanchez na Theo Walcot laki Wenger alisisitiza kwmba wamalizizji ndo wakulaumiwa na sio ubora wa Fabianski.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni