STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 12 Mei 2015

NGASSA AMWAGA WINO FREE STATE, SOMA ALICHOSEMA



KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa ' Anko' leo amesaini mkataba wa miaka minne (4) kuitumikia klabu ya Free State Stars inayoshiriki ligi kuu Afrika kusini.
Ngassa amesaini mkataba huo baada ya kufikia makubaliano leo asubuhi.

“Sasa najiandaa kwa maisha mapya baada ya kucheza Tanzania kwa muda mrefu, hii ni changamoto mpya kwangu, mpira wa Afrika Kusini upo juu sana ukilinganisha na pale kwetu (Tanzania). Nataka kutumia fursa hii kuitangaza soka ya Tanzania, ili klabu zisijifikirie tena kusajili wachezaji wa Tanzania,”amesema Ngassa asubuhi ya leo nchini Afrika kusini baada ya kusaini mkataba wa miaka 4 kuichezea timu ya Free State inayoshika nafasi ya 9 katika ligi kuu nchini humo.


Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa timu hiyo maarufu kama Ea Lla Koto, Mmalawi Kinnah Phiri amesema kwamba amekuwa akimpenda Ngassa kwa muda mrefu na kukutana naye FS ni kutimia kwa ndoto zake za kufanya kazi na kijana huyo siku moja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox