LUKAS
Podolski, mshindi wa kombe la dunia akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani
mwaka jana nchini Brazil ambaye kwasasa yupo kwa mkopo Inter Milan
kutokea Arsenal amehojiwa kuhusu mtoto wake na kufichua kuwa anazivutia
klabu nyingi.
Mtoto huyo mwenye miaka 7 anayeitwa Louis Podolski,
kwasasa yupo katika kituo cha watoto cha Bambini cha Inter na Podolski
ametangaza kuwa klabu tatu za Ujerumani zinajaribu kuiwinda saini ya
mtoto wake ili ajiunge na timu zao za vijana.
Timu hizo ni Cologne, Bayer Leverkusen na Borussia Mönchengladbach.
Podolski amesema: "Mtoto wangu sasa ana miaka 6 kuelekea saba, anaichezea Bambini (Inter). Tayari ameshanasa kwenye rada. Sasa Cologne, Leverkusen na Gladbach wanahitaji kumsajili. Katika umri huu, inashangaza!"
Podolski
alijiunga kwa mkopo na Inter katika dirisha dogo la usajili mwezi
januari mwaka 2014 na anatarajia kurejea Arsena mwishoni mwa msimu huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni