Taarifa
kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya klabu ya Azam fc zinaeleza kuwa
kocha wa zamani wa klabu hiyo, Muingereza Stewart John Hall anarejea
tena kuwa kocha mkuu.
Hall
aliyeiacha Azam fc baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi
kuu msimu wa 2013/2014 anarejea kuchukua mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu,
Joseph Marius Omog.
Omog
alifukuzwa kazi mwezi februari mwaka huu baada ya Azam kutolewa ligi ya
mabingwa Afrika na El Merreick kwa ushindi wa jumla wa magoli 3-2 na
nafasi yake ikachukuliwa kwa muda na aliyekuwa kocha msaidizi, George
'Best' Nsimbe.
Kwasasa
Nsimbe ndiye kocha mkuu wa muda na msaidizi wake ni Dennis Kitambi,
hivyo kurejea kwa Hall kuna maanisha kocha mmoja anaweza kuwa msaidizi
wake.
Nsimbe ameshindwa kutetea ubingwa aliochukua Omog msimu uliopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni