PICHA
yenye mvuto ilitawala katika mitandao ya kijamii wakati wa kipindi cha
kwanza cha mechi ya marudiano ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani
Ulaya baina ya Real Madrid na Juventus jana uwanja wa Santiago
Bernabeu.
Cristiano
Ronaldo iliifungia Real Madrid goli la kuongoza kipindi cha kwanza kwa
mkwaju ya penalti kufuatia James Rodgriguez kuangushwa kwenye eneo la
hatari na Giorgio Chiellini.
Baada ya faulo ya Chiellini wachezaji wa Juve walimzonga mwamuzi wa Sweden, Jonas Eriksson wakijaribu kupinga maamuzi yake.
Wakati wa tukio hilo, mpiga picha mmoja mjanjamjanja alipiga picha iliyoonesha kama golikipa wa Juventus, Gigi Buffonwas alikwenda kumbusu mdomoni mwamuzi Jonas Eriksson.
Tukio hilo lilirudisha nyuma kumbukumbu za watu kuhusu ishu waliyowahi kufanya Gary Neville na Paul Scholes enzi hizo wakiwa Manchester United.
Picha hiyo ilisambaa kwa haraka kwenye mitandao ya kijamii, cheki picha yenyewe hapo chini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni