Kocha
wa Real Madrid, Rai wa Italia, Carlo Ancelotti sasa amekuwa na
matarajio ya kutopata au kupoteza kibarua chake kuifundisha Real Madrid.
Akizungumza kupitia kituo cha Sky Sports mapema baada ya filimbi ya mwisho, Ancelotti alisema
"
Sijui, tuna siku 15 sasa kwaajili ya maandalizi ya mechi 2 zilizobakia
za ligi kisha tunamaliza msimu na kisha mazungumzo na klabu
yatafuatia''.
"
Suala la kuongelea hatima yangu na klabu sio la kujadili hivi sasa,
inabidi tumalize msimu vizuri iwezekanavyo" alizidi kusema.
"Tulipoteza
katika mchezo wa awali, wachezaji wetu walicheza vizuri sana lakini
hatukuwa na bahati, tulifanikiwa kupata nafasi nyingi sana lakini
tulikosa kuzitumia"
"
Ni vigumu kusema, timu ilifanya kila kitu kilichopaswa kufanyika,
tukishambulia sana lakini hatukuwa na bahati, kama ni kujilaumu basi ni
ile mechi yetu ya awali kule Turin"
"
Mpira ni maelezo madogo, mwaka jana tulishinda na tunashukuru kwa goli
la dakika za mwisho na kila mtu alisema ilikuwa bahati na hatua hii
hatukuwa na bahati kabisa ila yote kwa yote najisikia vyema juu ya
wachezaji hawa"
Katika
mchezo huo pia kiwango cha Gareth Bale bado hakikuwa kile kizuri kama
ilivyozoeleka pindi anapokuwa yupo na ari nzuri ambapo Ancellot hakusita
kumzungumzia na akisema
"
Alicheza vizuri, alijituma sana kwa bidii kama timu nzima ilivyofanya,
tulionesha kile tulichokiandaa lakini haikuwa nafasi yetu ya kufika
fainali" Muitaliano huyo alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni