Mechi ya kwanza Camp Nou, Barcelona walishinda 3-0 na jana usiku wakali hayo wa 'Katalunya' wamekufa 3-2 dimba la Allianz Arena mjini Munich.
Magoli ya Bayern yalifungwa na Mehdi Benatia dakika ya 7', Roberto Lewandowski 59' na Thomas Muller dakika ya 74, wakati nyota wa Brazil, Neymar Jr alifunga magoli yote mawili ya Barcelona dakika za 15' na 29' akipokea pazi zote kutoka kwa Luis Suarez.
Ukiachana na matokeo, soka lilikuwa zuri, Bayern walijitahidi kupambana na kumiliki mpira kwa asilimia 54 dhidi ya 46, lakini Barcelona si timu ya kuisogelea kirahisi.
Bayern walifika langoni kwa Barca na kupiga mashuti 8 yaliyolenga lango wakati wageni wao walipiga matano (5) tu.
Kitu cha kushangaza, Barca hawakupiga shuti lolote ambalo halikulenga lango, lakini Bayern waliokuwa na papara walipiga mashuti 10 yasiyolenga lango.
TAKWIMU ZA MECHI YA BAYERN v BARCELONA JANA
tatistics :
8
shots on target
5
10
shots off target
0
54
possession (%)
46
5
corners
1
3
offsides
3
19
fouls
14
5
yellow cards
2
1
goal kicks
Leo usiku majira ya saa 3:45 Real Madrid wanaikaribisha Juventus 'Vibibi vya Turin' katika mechi ya marudiano ya nusu fainali inayopigwa uwanja wa Santiago Bernabeu.
Mechi ya kwanza uwanja wa Juventus mjini Turini, Real walikufa 2-1 na leo wanahitaja ushindi wa goli 1-0 ili kutinga fainali kwa faida ya goli la ugenini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni