Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro (katikati) leo akiwa makao makuu ya klabu hiyo Jangwani, amemtambulisha rasmi kiungo wao mpya wa ushambuliaji, Deus Kaseke (kulia) ambaye jana alisaini mkataba wa miaka miwili kuwachezea mabingwa hao wa Tanzania bara .
Kaseke aliyekuwa anakipiga Mbeya City misimu miwili iliyopita amekabidhiwa jezi namba 4 aliyokuwa anaitumia pia kwa Wagonga nyundo wa Mbeya.
Swali ni je, beki Rajab Zahir aliyekuwa anavaa jezi hiyo ataondoka au atapewa jezi nyingine?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni