Didier Drogba amesema kamwe hawezi kucheza timu nyingine yoyote ya ligi kuu nchini Uingereza wakati huu anapoachana na klabu yake ya Chelsea.
Taarifa zilizopo zinadai kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa Didier Drogba kuungana na Frank Lampard pamoja na Steven Gerrard kuelekea nchini Marekani kukipiga katika ligi kuu nchini humo.
"Kiukweli kuna timu nyingi sana nzuri ligi kuu nchini Uingereza lakini mapenzi yangu kwa timu hii...siwezi kuchanganya na timu nyingine ya EPL.
"Tangu nilipotangaza mitandaoni kuwa naondoka Chelsea, wakati nipo katika vyumba vya kubadilishia nguo, nilipokea simu kutoka timu mbalimbali ambazo nyingine zilinipa mshangao kabisa.
"Hii inaonesha labda naweza kufanya kitu kwa timu. Bila shaka navutiwa pia na USA," Aliongeza Drogba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni