BOSI wa Bayern Munich, Pep Guardiola amemtaja Lionel Messi kuwa ndiye 'mchezaji bora wa wakati wote'.
Guardiola ametoa kauli hiyo baada ya timu yake kutupwa nje ya UEFA kwa kipigo cha jumla cha magoli 5-3 dhidi ya Barcelona.
Mechi ya kwanza kocha huyo wa zamani wa Barcelona alikufa 3-0 Camp Nou na jana usiku ameshinda 3-2.
Messi amecheza kwa kiwango cha juu katika mechi zote mbili na kumfanya Guardiola ashindwe kuzuia hisia zake.
"Ni
mchezaji bora wa wakati wote,' Guardiola amesema. "Namfananisha na
Pele. Ninafurahia sana kuona mpira wa aina hii". Amekiri Guardiola.
Nyota
huyo ambaye anafurahia msimu mzuri Barcelona na ameshafunga magoli10
katika mashindano ya ulaya, juma lililopita aliwafumua Bayern katika
kipigo cha kwanza cha mabo 3-0 Camp Nou akifunga mara mbili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni