STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 28 Mei 2015

JAHAZI LA FIFA KUHUSU UCHAGUZI WA KESHO (MR GOLDEN VS CHOI)

MR'GOLDEN vs MR'CHOI 

MR'GOLDEN-Oya haina kulemba ngoja tuone nani ni sahihi maana kuna vitu huwa unajifanya mbishi sana vingine sio vya kubisha. 
 
MR'CHOI-Ah we jamaa bhana sasa unahisi wewe utakuwa sahihi aya sasa mwaga mchele mchangani tuuchambue alafu mwisho wa siku tuone. 

MR'GOLDEN-FIFA hili ni shirikisho la soka la kimataifa Duniani ambalo limekuwa likisimamia maswala yote ya Kandanda Duniani likiwa limeanziswa rasmi mwaka 1904 na Rais wa kwanza wa shirikisho hilo alikuwa Mfaransa Robert Guerin aliye dumu mpaka 1906 kisha akamuachia Daniel Burley Woolfall wa visiwa vya Malkia 1906-1918 kisha kina Jules Rimet Ufaransa 1921-1954,Rodolphe Seeldrayers Ubelgiji 1954-1955,Arthur Drewry Uingereza 1955-1961,Sir Stanley Rous Uingereza tena 1961-1974,Dr João Havelange Brazil 1974-1998 kisha akachukua madaraka king'ang'anizi wa Uswisi Sepp Blatter kwanzia 1998 mpaka sasa. 

MR'CHOI- Sawa tunajua tuende kwenye lengo lenyewe maana utanichosha na hivyo vihistoria mwishoe nikose hamu ya kujadili alafu tusogee chini ya mti Jua lisha kuwa kali muda wa kufika Jahazi bado. 

 MR'GOLDEN- Sepp Blatter amekuwa Rais wa FIFA kuanzia mwaka 1998 ,katika chaguzi zote 4 alizogombea Blatter amekuwa akishinda huku kukiwa na mambo mengi yakisemwa ikiwa ni pamoja na skendo za rushwa safari hii Blatter yupo tena kwenye Kinyang'anyiro cha kugombea urais wa FIFA kwa mara ya 5. 

MR'CHOI- Ndio yupo kama kawa utu uzima dawa hizo skendo ni kawaida hakuna sehemu isiyo na kasoro mbalimbali hata katika familia yako kuna kasoro kikubwa ni kuzipunguza maana hata kuzifuta pana ugumu China yenyewe huwa wananyonga ila jiulize bado watu wanapokea rushwa . 

MR'GOLDEN-Aaaa..wacha niseme,Blatter FIFA pamemshinda,Nasema pamemshinda huku tukihitaji kuona viongozi wapya wakiingia madarakani ili kubadili au kuboresha Kandanda ili uwe mchezo wa kisasa zaidi Blatter ni kama Dikteta anayetaka kuendelea kuiongoza FIFA kimabavu ili hali FIFA pakiwa pamemshinda.Narudia tena FIFA pamemshinda... 

 MR'CHOI- We rudia tena ikiwezekana tunga kabisa wimbo ila hatoki mtu eti dikteta kwa lipi sasa maana huwa uchaguzi unafanyika na anashinda kihalali ustake kuwaiga wa Libya ambao ''walifurahia supu ya pelege wakajuzwa kuongezewa supu ya pweza matokeo yake hivi sasa hata hiyo ya pelege hawaioni achilia mbali ya pweza wamebaki kunywa supu ya dagaa.'' 

MR'GOLDEN-We jama bhana hivi unakumbuka Mwaka 2014 wakati wa kombe la Dunia Brazil ,MR.RAY WHELAN ambaye ni meneja mkuu mtendaji wa kampuni ya mshiriki wa FIFA,"Match Hospitality" alikamatwa ktk hoteli moja huko Rio De Jeneiro iliyokuwa ikitumiwa na maafisa wa shirikisho la FIFA kwa kujihusisha na vitendo vya uuzaji wa tiketi za kombe la Dunia kinyume na Kanuni.Blatter alichukua maamuzi gani ya maana katika hili? 

MR'CHOI-......ah,ammmm eee aaah bhana e hapo alikuwa bize na majukumu ila..? 

MR'GOLDEN- Na bado ujashikwa na kigugumizi Wacha nikukumbushe hili,Rais wa UEFA Michael Platini wakati anajitoa kwenye kinyang'anyiro cha urais wa FIFA mwaka 2014 alisema,"Utawala wa Blatter hauwezi kuwa mzuri kwa maendeleo ya Soka" .Hii inaonesha ni jinsi gani FIFA pamemshinda Blatter. 

MR'CHOI-Kumbe alisema tu pasipo ushahidi alafu kama kweli alikuwa mpambanaji kwa nini alijitoa.? angepigana mpaka mwisho tuone watu wengine bhana. 

MR'GOLDEN-Ushahidi upu kwani aliwahi kuitwa kwenye kamati ya maadili ya FIFA(2014) ili kuchunguzwa kuhusiana na Kashfa za rushwa ,kwa maajabu na kutokujitambua kwa Kamati ya maadili ilisema Sepp Blatter alikuwa hana Kesi ya kujibu na hapa ndipo tunapoona madudu ya Rais Sepp Blatter na Kamati yake. 

MR'CHOI- Kweli kuna watu wana matatizo ya ufikiri sasa kamati haikupata makosa dhidi yake ulitaka iweje basi unda wewe kamati au hao mnaomkashifu mka mchunguze tena maana kuna watu mnajifanya kuchonga tu kumbe ndo walewale. 

MR'GOLDEN-Sasa wacha nikurudishe nyuma kidogo,Mwaka 2011 Makampuni makubwa ya Coca Cola na Adidas ambayo ni wadhamini wakubwa wa FIFA ,yalionesha kusikitishwa na tuhuma za rushwa zinazotolewa na FIFA ,Lakini Rais Sepp Blatter alikanusha kashfa hizo bila kuzifanyia uchunguzi wa kina. Je,Tukisema FIFA pamemshinda Blatter tunamkosea heshima yake?? 

MR'CHOI-Hapaja mshinda na mnamkosea heshima yake. 

MR'GOLDEN-Aiseee......amini usiamini,Blatter FIFA pamemshinda tena ni wakupiga mawe anatuharibia soka tuhuma za hongo ktk uenyeji wa kombe la Dunia la Mwaka 2018 Urusi na 2022 nchini Qatar ziliibuka ndani ya uongoz huu- huu wa Blatter tena mpaka hongo za saa zenye thamani ya Dola 25,000 kwa wajumbe wa kamati ya utendaji Choi kwanini tusiseme Blatter ni Dikteta asiyetaka kujiuzulu? we niaje..? 

MR'CHOI- Tena hapo ndo usiguse kabisa hata kama ila lazima apewe heshima yake kwa kulieneza soka la kimataifa Duniani kote na ndo maana tukalishuhudia Asia 2002 likaja kwetu 2010 we unadhani pasipo yeye ni lini tunge shuhudia kombe la Dunia katika mabara yote.? Acha ukuda wewe jamaa sio mbinafsi na ndio kiongiozi bora anapaswa kuwa kina Cameroon kimewachoma kukosa nafasi na ndomaana wakaingiza bifu zao za kisiasa na Urusi kutaka asepe madarakani kisa wametoswa hivi wewe hufikirii unadhani uwenyeji wa kombe la Dunia angepewa Uingereza ungesikia maneno ya kumkashifu...? 

MR'GOLDEN- Ila kumbuka tuhuma zimeanza kitambo tu usikurupuke Kama hiyo haitoshi,mapema wiki hii Maafisa zaidi ya 14 wametuhumiwa kupokea rushwa na kati ya hao tisa wapo madarakani sita walikamatwa katika hoteli moja mjini Zurich nchini,Switzerland. kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa ya takriban kiasi cha dola za Marekanimilioni 100 kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20. 

MR'CHOI-Dah unakurupuka vibaya kumbuka hao maafisa walio kamatwa walikuwa chini ya uongozi wa Mbrazil Dr João Havelange 1974-1998 maana wametenda makosa kipindi cha mwaka 1990 wakati huo Mzee wetu Blatter alikuwa katibu mkuu 1981-1998 na kwa taarifa yako alikuwa anajua swala hilo ndo maana haja shangaa na anaunga mkono harakati zote za kuwafagia wala rushwa na hii imedhihirisha ni kiongozi bora kwa kutowakingia kifua. 

MR'GOLDEN- Ukweli ni kwamba Rais Sepp Blatter hana sifa ya kuendelea kuwa rais wa FIFA kutokana na Mlolongo wa Kashfa za rushwa unaomkabili kwa heshima ya soka ,Blatter anatakiwa kujiuzulu au kuondolewa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Urais ili kurudisha hesima ya mchezo huu unaopendwa na watu wengi Duniani mimi hunielezi kitu wewe. Alafu skia wewe dogo.... 

Wakati LUIS FIGO anatangaza nia ya kugombea Urais wa FIFA alisema,"Naangalia heshima ya FIFA kwasasa siipendi,soka linastahili uzuri.Katika wiki,miezi na hata miaka ya hivi karibuni ,nimeona taswira ya FIFA ikiporomoka.Baadae LUIS FIGO aliamua kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kulalamikia mfumo wa uendeshaji wa uchaguzi huo na kuuita kuwa ni wakinafiki. Naye rais wa chama cha soka huko Uholanzi MICHAEL VAN PRAAG aliamua kujitoa kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa FIFA baada ya kuona mfumo wa uendeshaji wa uchaguzi hauko sawa. 

MR'CHOI- Oya mbona unaongea mfululizo naona umepaniki dadeki utapiga deki hapa alafu huyo alie jitoa hasahasa huyo Figob bora alisepa maana angeaibika mtu katoka kuwa balozi wa nyumba kumi alafu anataka kuwa raisi kwa misingi gani labda yani nampongeza aliemshauri akajiudhuru , hao wengine nao sikuona jipya kwao wasepe tu.

 MR'GOLDEN-Hakika Blatter amejijengea ukuta ambao ni vigumu sana kumuondoa madarakani kwa njia ya uchaguzi huo ndo ukweli na Kwasasa wamebaki wagombea wawili,Sepp Blatter ambaye ni rais wa sasa wa FIFA na PRINCE AL HUSSEIN ambaye ni mwanachama wa kamati ya FIFA. Tunahitaji kiongozi mpya atakayepambana kwanza na hizi kashfa za rushwa zinazoibuka kila kuitwapo leo kwenye shirikisho la soka duniani FIFA ili kuufanya mchezo wa soka uendelee kuwa na ladha tunayoitaka wanasoka wengi yote kwa yote Blatter hastahili kuendelea kuwa rais wa FIFA. 

MR'CHOI-Yamewashinda ya vyama vya soka kwenye Wilaya zenu uje mpaka ngazi ya Mkoa achilia mbali ya Taifa mtayaweza ya Fifa wewe na hao pigeni tarumbeta wee ila hata hapo mpaka wa Kenya hayafiki wajua tatizo lenu mmesha kopi tabia za waleee wanao waleteaga misaada mwenye akili timamu akichunguza atajua kuwa kosa la Blatter ni sera zake za usawa kwenye mpira Duniani kote. 

Hata kama kuna tuhuma isiwe chanzo cha mkashifu kwanza huyo chambo Prince Al Huusein hamna kitu kabisa pigeni debe tu huyo Platin alivyomnafki anasukumia wenzake si ajitokeze yeye.

MR'GOLDEN- Poa ngoja tuone ila ukweli umejulikana jahazi lile ubishi uishe tutatupana majini bure, tusepe

MR; CHOI- Poa ila najua wakati wa matokeo, utapita kushoto mimi kulia cha msingi usinikimbie turudi wote huu mchele ngoja ndege waje kula

KWA MAONI 
Choikangta.ckt@gmail.com
 titusdickson1@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox