Safari tunaianza ingawa imeanza mapema ila ndo hivyo si unajua sisi wazee wa zamani mambo yetu huwa tunayapangilia mapema sana waswahili tunasema cheleachelea utakuta mwana si wako. Kikubwa ni kuangazia wana fainal wa msimu huu pamoja na vidodoso vya mkongwe Paul Maldin.
Kama ambavyo tunajua ligi nyingi zilianzishwa miaka mingi iliyopita tangu enzi zile za nchi nyingi za bara la Afrika zikiwa ni makoloni.
Hapa tutajikita katika kombe la mabingwa Uefa vidodoso vya zamani na kuanzia 1992 mwaka ambao umebeba mengi ya kimichezo kwa maana mabadiliko ya ligi nyingi yalianzia hapo.
Hatuwezi anza safari pasipo wimbo maana ni ndefu tena kama kawa wimbo wa safari hii ni ule ulio andikwa na muingereza Tony Britten wa Uefa usisahau mzaliwa wa Bern-Uswiss Jong Stadelmann ndie mbunifu wa kombe hili.
Maldin- wajua hili ni miongoni mwa makombe yanayo sisimua wapenda soka kutokana na ushindani chagizo ni ushiriki wa vilabu bingwa Ulaya ambavyo kwa namna moja ndivyo vilivyo shika hisia za mashabiki wengi Duniani na kikubwa mpira wa Ulaya ndio jicho katika mchezo wa soka.
Choi- Kweli wajua mpira umesambaa Duniani kote isipo kuwa wa Ulaya una ukamilifu katika engo zote tofauti na huku kwetu tunalipeleka ilimradi lina enda.
Maldin- Tambua kuanzishwa kwake 1955 Real Madrid waliweka historia ya kuchukua mara tano mfululizo yani mwaka 1956, 1957,1958,1959,1960 katika mfumo mpya 1992 hakuna timu iliyo wahi kutetea ubingwa huu.
Choi- Mh sasa hapo walifanya lao maana na hili wamezidi liendeleza hadi kwenye nyanja tofauti wamekuwa ni vinara kwanzia utajiri mpaka usajiri wa wachezaji kwa dau kubwa pia kwa namna ya mfumo huu mpya hakuna alie tetea hivyo inadhihirisha kwa sasa kuna ushindani mkubwa kuliko kabla.
Maldini- Utajiri lazima wawe nao pia tambua ni vilabu 22 pekee ndivyo vilivyo bahatika kuchukua ubingwa huu kwa maana hiyo kombe hilo limenyanyuliwa mara 59, vinara wa kulibeba ni Real Madrid wamechukua mara 10,Ac Milani-7, Liverpool-5,B.Munich-5 ,Ajax-4 sawa na Barcelona hizo ndizo timu zilizo chukua mara nyingi zaidi.
Choi-Kwa maana hiyo Barcelona wanatafuta ubingwa wao wa 5 na kumbuka Juventus wamechukua mara 2 hivyo wata tafuta ubingwa wa 3 kuwa sawa na Manchester United na Inter Milan. Maldin- Ukiangazia orodha yote kwa ujumla tangu mfumo wa zamani vipo vilabu ilivyo potea katika anga hili ni Redstar,Notigham forest, Aston Villa na Hamburg.
Choi- Ni kweli ila kuna vilabu vimekuwa wanafamilia wa kombe hili kwa maana wameshiriki mara nyingi zaidi hapa tunawazungumzia Real Madrid,Barcelona,Bayern munich NK.
Maldin- Uhispania ndipo kombe limetua mara nyingi zaidi 14 zikifuata nchi za Italia na Uingereza mara 12 kwa maana hiyo Barcelona watahitaji kupandisha takwimu za taifa la Hispania kuchukua mara ya 15 na Juventus watahitaji kuwakimbia Uingereza na kuwakaribia Hispania kwa kuchukua mara ya 13.
Choi- hayo ni machache yalio angaziwa kwenye kombe hilo nadhani mimi na mkongwe wangu ngoja tuvute pumzi safari bado ni mbichi . ITAENDELEA - KESHO 27/5/2015KWA MAONI:: Choikangta.ckt@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni