Kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Stand United, ndiyo kimeishusha Ruvu Shooting hadi daraja la kwanza.
Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amekubali kipigo lakini akasisitiza: “Ilikuwa utafikiri hawako Tanzania.”
“Walikuja
vijana na mapanga hadi hotelini kwetu, walitutishia. Ikafikia
tukashitaki kwa mabosi wa polisi lakini hakuna aliyetusaidia.
“Nikalazimika kuwasiliana na kuwasiliana na makao makuu ya Polisi kupitia Chagonja, ndiyo tukapata msaada.
“Lakini tulipoingia vyumbani, mambo yalikuwa mazuri. Tulipotoka kwenda kupasha mwili, kosa kubwa.
“Tumerudi
vyumbani kuna harufu kali ya dawa iliyopuliziwa kwa ajili ya kupunguza
nguvu ya mwili. Hii imechangia kwa kiasi kikubwa kuwaumiza vijana.
Kamisaa ameona, nimemuita na harufu kaivuta pia, waandishi wameona.
“Achana
na hivyo, tulipambana sana uwanjani lakini mwamuzi alikuwa kama ni mtu
aliyepewa maagizo kwamba sisi lazima tufungwe,” alisema Masau ambaye
timu yake itacheza daraja la kwanza msimu ujao.
Chanzo:Salehe Jembe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni