Paul
Pogba amerudi kwa kasi kutoka majeruhi na kutupia goli lililoipa sare
ya bao 1-1 timu yake ya Juventus dhidi ya vibonde wanaopigania kutoshuka
daraja timu ya Cagliari jana Jumamosi.
Kocha
wa Juve Massimiliano Allegri alipumzisha takribani nyota wake wote kwa
ajili ya mchezo wa klabu bingwa dhidi ya Real Madrid, utakapoigwa katika
dimba la Santiago Bernabeu.
Kiungo wa Juventus Paul Pogba akijinyoosha kuupiga mpira ambao ulizaa goli la pekee kwaJuve jana.
Goli la Cagliari lilifungwa na Luca Rossettini.
Gianluigi
Buffon, Giorgio Chiellini, Leonardo Bonucci, Stephan Lichtsteiner,
Fernando Llorente na Alvaro Morata wote hawa walianzia benchi.
Kiungo
mchezeshaji mkongwe wa timu hiyo, Andrea Pirlo alikuwa jukwaani kabisa
kuangalia pambano hilo pamoja na mfungaji bora wa klabu hiyo kwa sasa
Carlos Tevez.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni