MOURINHO AWEKA NGUMU, ASEMA PETR CECH HATOKI LABDA VINGINEVYO, SOMA HAPA.
Jose Mourinho ametamka hadharani kuwa atapinga kwa nguvu zake zote kuuzwa kwa mlinda mlango wa timu hiyo Petr Cech wakati
dirisha la usajili litakapofunguliwa hasa kwa vilabu pinzani kama
Arsenal, lakini akasisitiza kwamba yeye si mwenye maamuzi ya mwisho
klabuni hapo.
“Jose
Mourinho ni kitu kimoja, na Abramovich ni kitu kingine, Pia kingine ni
bodi sababu, bodi ipo kati yangu mimi na watu wengine pia,” Mourinho
alisema.
“Kama
ingekuwa ni mimi, na maamuzi yangu, ningetaka Petr abaki hapa. Hivyo
tu. Ingekuwa ni maamuzi yangu basi Petr angebaki.” Hata kama ni kinyume
na matarajio yake? “Ndio.”
“Nadhani
klabu ni muhimu zaidi ya mchezaji na kama ilivyokuwa msimu huu, klabu
ilihitaji makipa wawili ambao ni bora kabisa,” Mourinho aliongeza. “Bila
ya Petr msimu huu sidhani kama tungekuwa mabingwa kwa sababu alicheza
michezo sita ambayo ilikuwa ni muhimu sana katika ligi.
“Kwangu
mimi, uamuzi wa kwanza, ni Petr kubaki. Baada ya hapo sasa, uamuzi
mwingine ni kwamba aende lakini sio abaki hapa Uingereza. Kitu
nisichokitaka kwake ni yeye kubaki hapa katika klabu za Uingereza. Ila
narudia tena, Mimi ni kocha na Cech ana maana kubwa sana kwangu na kwa
klabu hii, na alichokifanya klabuni hapa ni kikubwa sana, kama maamuzi
yangu yanatofautiana na klabu basi ntakubaliana nayo tu.”alimalizia
Mourinho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni