Pazia
la ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2014/15 limefungwa rasmi leo, ambapo
imeshudiwa timu za Ruvu Shooting na Polisi Moro zikishuka daraja baada
ya kupoteza michezo yao.
Kwa
kuanzia katika jiji la Mbeya, timu ya Mbeya City walikuwa
wakiwakaribisha Maafande wa Polisi Moro ambao hata hivyo walikuwa tayari
wameshuka daraja. Katika mchezo huo Mbeya City walishinda kwa bao 1-0.
Mkoani
Mtwara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, kulikuwa na pambano kali na
la kusisimua, ambapo Ndanda FC walikuwa wakiwakaribisha mabingwa wapya
wa ligi hiyo Yanga SC na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Matokeo hayo yamezua shangwe na vifijo kwa Ndanda baada ya
kijihakikishia nafsi yao ya kubaki ligi kuu kwani endapo wangepoteza
mchezo huo basi wangeshuka daraja moja kwa moja.
Katika
uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, ilikuwa ni patashika nguo
kuchanika pale Stand United walipokuwa awanawakaribisha Ruvu Shooting,
matokeo ya mchezo huo ni kwamba Stand waliibuka na ushindi wa goli 1-0
kwa bila na kunusurika kushuka daraja, huku Ruvu Shooting wao
wakiteremka daraja.
Huko
Manungu Complex katikati ya mshamba ya miwa, Mtibwa walikuwa
wakiwakaribisha Wagosi wa Kaya Coastal Union, ilishuhudiwa timu hizo
zikitoshana nguvu kwa kufungana goli 1-1 na hata hivyo timu hizo kusalia
katika ligi kuu msimu ujo.
Nao
Tanzania Prisons ya Mbeya na Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera
walitoshana nguvu kwa kutoka suluhu, mchezo huo ulipigwa katika dimba la
CCM Kirumba jijini Mwanza. Matokeo hayo yameinusuru Prisons kushuka
daraja na kusalia ligi kuu kwa msimu ujao.
Nako
katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam, timu ya JKT walikuwa
wanawakaribisha Wekundu wa Msimbazi Simba Sc na kushuhudia Simba
wakiibuka na ushinda wa magoli 2-1. Mchezo huo ulikuwa hauna athari
yoyote kwa timu zote mbili, hivyo kusalia ligi kuu.
Kwenya
uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es
Salaam, Azam Fc waliwakaribisha vijana wa Mgambo JKT kutoka jijini Tanga
na kushuhudia timu hizo zikitoka suluhu.
Timu ambazo zimepanda ligi kuu kwa msimu ujao ni Mwadui FC, Majimaji, Toto Africans na African Sports.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni