Kutoka katika jarida la Daily Telegraph linaripoti kwamba mshambuliaji tokea klabu bingwa mtetezi ligi kuu ya Hispania Atletico Madrid Antoine Greezman tayari ameshafungua milango ya kwenda Chelsea.
Nyota huyo huyo kwa mujibu wa klabu yake wanamtaka kuongeza mkataba lakini yeye bado anasubiri kusikia Chelsea watasema nini hapo baadae.
Kwa upande mwingine pia wakala wa mchezaji Angel Dimaria kutoka Manchester united George Mendez amesema kwamba yupo katika mazungumzo na klabu ya PSG ili wamnyakue nyota huyo.
Wakala huyo alikutana na timu hiyo mara ya mwisho wakati PSG walipokutana na Fc. Barcelona katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya mnamo mwezi wa 4 mwaka huu. Gazeti la Daily Express linaripoti.
Daily Mail nao wanaripoti kuwa Luis Enrique yuko katika katika mipango ya kuondoka Fc. Barcelona hata kama akishinda Kombe la ligi mwaka huu.
Enrique (45) hadi sasa ananyemelewa mabingwa watetezi wa ligi ya Uingereza Manchester City.
Nayo klabu ya Juventus imekataa tenda ya kitika cha paund mil 80 ilimchukue nyota wake mdogo Paul Pogba itakapofika mnamo mwaka kesho January 2016 na badala yake wanahitaji pesa zaidi kwani iliyotajwa no ndogo, jarida la Tuttosport linaripoti.
Gareth Bale anaweza kuifanya Manchester United kutumia kitita cha Paund mil 275 kufuatia usajili mwingine wa Memphis Depay katika msimu huu wa majira joto.
Jarida la Daily Express linaripoti uwezekano mkubwa upo wa Bale kujiunga na United haswa kutokana na msimu huu kutokuwa mzuri akiwa na Real Madrid.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni