Jose Mourinho amesema kuwa, ni Lionel Messi ambaye ndio ameifanya Barcelona kuwa timu ya kuogopwa na wala si kocha wa zamani wa timu hiyo Pep Guardiola, na kusisitiza kamwe nyota huyo hataondoka klabuni hapo.
Alipoulizwa kama angependa Chelsea wacheze kama ambavyo Barcelona au Bayern Munich, Mourinho akasema: “Watu wanakosea sana. timu ni kitu kimoja. Halafu kitu kingine ni timu ambayo ina Messi ndani yake. Ni hadithi tofauti hiyo. Alicheza fainali ya ligi ya mabingwa akiwa na Frank Rijkaard. Alicheza vivyo hivyo pia akiwa na Guardiola. Na pia atacheza fainali akiwa na Luis Enrique. Na ikiwa siku moja akicheza akiwa chini ya Anthony [jina la asili ya kireno], basi huyo Anthony naye atafika fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya. Sasa basi, watu wanatakiwa kujua tu kwamba wanavyoichambua ile timu, basi wakumbuke kwamba huyu mtu ndio anayeleta utofauti wa kila kitu.”
“Messi yeye kama yeye analeta tofauti kubwa sana,” Mourinho alisema. “Hivi una shaka yoyote kwamba Man City ikiwa na Messi wanaweza kushinda klabu bingwa? au Arsenal yenye Messi inaweza kushinda ligi ya mabingwa? au Chelsea yenye Messi inaweza kushinda ligi ya mabingwa?Au Man United yenye Messi inaweza kushinda ligi ya mabingwa? Mimi nadhani hivyo. Sisemi kwamba mara zote hushinda. Namaanisha kuwa timu yenye yule kiumbe lazima itakuwa timu tofauti tu, na hadithi nyingine.”
Mourinho safari hii amekuwa katika hali isiyo ya kawaida huku akiwa ametolewa mapema kabisa katika michuano hii, lakini akasema kuwa burudani yake ilikuwa ni kumuangalia Messi.
• Sahau kuhusu takwimu - Messi na maajabu yake ni pambo linalopendezesha mpira
“Kumuangalia Messi, hautalaumu kuwa pale,” aliongeza. “Unafurahi kiasi ya kwamba haufikirii kutokuwepo pale. Unafikiri tu anachokifanya. Kila wakati nilivyocheza dhidi yake nilitumia masaa mengi sana kumsoma kiundani jinsi ya kumdhibiti. Na mara nyingi tulifanikiwa. Na mara nyingine pia tulishindwa.
“Nilipokuwa Inter, tuliweza kumzuia katika michezo yote. Njia nzuri ya kumdhibiti ni kucheza naye kwa karibu (man to-man), hiyo ni nzuri kuliko kumhusisha kila mtu.
Unapofanya hivyo unaenda kwa nguvu ile ile, japokuwa mfumo huo kwake pia bado ni shida. Nimecheza dhidi yake mara nyingi sana. Na kila muda nilikuwa nafikiria namna gani nitamzuia – Sisemi kumzuia kwa maana ya kumzuia–ni kumpa tu wakati mgumu. Hicho ndicho kitu nafuu unachioweza kumfanyia,”
Je ipo siku Messi ataondoka Barcelona? “Kwa maoni yangu mimi, sioni kama kuna hiyo nafasi,” alisema Mourinho. “Klabu kubwa kama ile, yenye nguvu namna ile, hawawezi kukubali kupoteza nguzo kama ile, yule ni wa pale tu, anamilikuwa na watu wa pale. Japo katika huwezi jua nini kitatokea, lakini siamini katika hilo.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni