Manny Pacquiao amepingana kwa nguvu zake zote na matokeo ya pambalo lake dhidi ya Floyd Mayweather Jr kuwa ameshindwa pambano hilo la welterweight.
Floyd Mayweather amemshinda Manny Pacquiao katika pambano hilo ambalo watu wengi wanadai kuwa maamuzi yalikuwa ni ya kutatanisha.
Pacquiao kwa upande wake anasema majaji watatu wa pambano hilo hawakutoa maamuzi sahihi
"Mimi nilidhani nimeshinda pambano, mimi sikuona kama Mayweather alifanya chochote kile kwangu, nilimpelekea makonde mara nyingi zaidi huku yeye muda mwingi akitumia kupanchi," Pacman alisemasaid. "Nilimshambulia mara nyingi zaidi."
Pambano hilo ambalo limepewa sifa kama pambano la karne lilifanyika katikaukumbi wa MGM Grand arena uliopo Las Vegas.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni