Goli La Kiungo Ramadhani Singano Limetosha Kuipa Point Tatu Muhimu Simba SC Katika Mchezo Wao Dhidi Ya Mabingwa Wa Msimu Uliopita Azam FC, Na Kupelekea Tofauti Ya Pointi Kutoka Nne Mpaka Kufikia Moja.
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Taifa Azam FC waliuanza mchezo kwa kasi, na kufanikiwa kutengeneza nafasi ambazo walishindwa kuzitumia.Kadri ya muda ulivyokuwa unaenda Simba SC walikuwa wanaingia mchezoni taratibu na kuanza kupokanya utawala wa mchezo toka kwa Azam FC.
Katika dakika ya 35 kiungo Salum Aboubakari alizawadiwa kadi nyekundu, ikiwa ni baada ya kupewa kadi ya pili ya njano, na kupelkea Azam FC kumaliza wakiwa pungufu.
Kutoka kwa Salum Aboubakari kuliipa Simba SC nguvu ya kushambulia, na kutawala mchezo na kupelekea kocha George Nsimbi kumtoa Franky Domayo na nafasi yake kuchukuliwa na Bryson Raphaeli.
Katika kipindi cha pili Simba SC waliuwanza mchezo kwa kasi na katika dakika ya 48 Ibrahim Ajibu aliiandikia Simba SC goli la kuongoza, kwa kichwa.
Kuingia kwa goli hilo kulizidi kuipa uimara Simba SC na kuifanya Azam FC kuwa nyuma muda mwingi na kupeleka mashambulizi ya kushtukiza.
Ilikuwa dakika ya 57, Mudathir Yahya aliisawazishia Azam FC goli na kuirudisha mchezoni Azam FC.
Alikuwa Ramadhani Singano aliyeipa ushindi Simba SC katika dakika ya 74, na kupelekea mchezo kumalizika kwa simba kuibuka na ushindi wa goli 2-1 na kufikisha pointi 44 huku Azam FC wakiwa na pointi 45.a\
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni