Manny Pacquiao anatarajia
kufanyiwa upasuaji wa bega lake ikiwa ni siku chache tu baada ya kupoteza
pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather.
Imeelezwa kuwa bondia alipambana
na Mayweather huku akiwa na maumivu makali ya bega.
Lakini majibu ya kipimo cha
MRI baada ya pambano hilo, yameonyesha kuwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji.
Taarifa nyingine zimeeleza
kuwa Pacquiao alikataliwa kuchoma
sindano ya maumivu kabla ya pambano hilo.
Pia baadhi ya habari zimeeleza kwamba bondia huyo alikosa siku kadhaa za mazoezi kutokana na hali hiyo ya maumivu wakati akijiandaa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni