STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 24 Mei 2015

SIMBA YAJIBU MAPIGO KWA YANGA YAMTWAA MWALYANZI WA MBEYA CITY;

Mwalyanzi akisaini mkataba wake kwenye ofisi za Simba sc .      

WAKATI Yanga SC wakisherehekea saini ya winga Deus Kaseke, Simba SC nao wamefanya yao mchana huu.

Kiungo hodari mchezeshaji Peter Mwalyanzi kutoka timu ile ile, Mbeya City aliyotokea Kaseke amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na Wekundu wa Msimbazi.

Mwalyanzi moja ya viungo waliong’ara katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu ambaye alikuwa anamchezesha vizuri Kaseke, amesaini ofisini kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe, Mbezi, Dares Salaam.

Na Poppe aliyekuwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Collins Frisch akasema;

“Sisi tunajua wachezaji bora na Simba SC ndiyo nyumbani kwa wachezaji bora,”.

Poppe amesema kwamba Mwalyanzi ni pendekezo la kocha Mserbia, Goran Kopunovic lakini hata washauri wengine wa masuala ya kitaalamu wameridhishwa na uwezo wa mchezaji huyo.

Kwa upande wake, Mwalyanzi amesema kwamba anajisikia furaha kusaini timu hiyo kubwa, kwani ni hatua moja kubwa mbele katika maisha yake ya soka.

“Mchezaji yeyote anapokuwa anaibuka katika nchi hii, ndotozake ni siku moja kucheza timu kubwa kama hizi, na mimi nimefurahi sana kujiunga na Simba SC,”amesema.

Mwalyanzi ameongeza kwamba baada ya kusaini, anaomba ushirikiano kutoka kwa wachezaji wenzake, viongozi na mashabiki ili aweze kufanya vizuri.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox