Beki wa zamani wa
Barcelona, Eric Abidal ameamua kufungukam mambo mengi kuhusiana na uginjwa
wa kansa.
Pamoja na mengi,
ameendeleza jambo ambalo limewashitua wengi baada ya kusema beki mwenzake
wakati huo, Dani Alves alikuwa tayari kumzawadia moja ya ini lake.
Abidal raia wa
Ufaransa aliambiwa na ugonjwa wa kansa kwenye ini mwaka 2011 alipokwenda
hospitai kufanyiwa vipi vya kawaida.
“Sikujua kama
nilikuwa mgonjwa, nilikuwa fiti lakini ilikuwa ni kawaida kwenda hospitali na
kufanyiwa vipimo fulani baada ya muda fulani.
“Nikaambiwa ni
mgonjwa, hakika nilishituka sana. Lakini nikaanza matibabu.
“Wakati fulani, Alves
alisema alikuwa tayari kutoa ini lake kwangu.
“Lakini nikaona si
sahihi, lilikuwa ni jambo zuri lakini hapa kwa kweli. Sikukubaliana naye,”
alisema Abidal wakati akihojiwa na DailyMail la Uingereza.
Kwa sasa
anajishughulisha na Abidal Foundation inayofanya kazi ya kusaidia kuwatibu
watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kansa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni