Msuva ameondoka leo alfajiri lakini uongozi wa Yanga
umelalamika kutokana na mchezaji huyo kushindwa kuaga na kujiondokea
pasipo ruhusa
Msuva ameondoka leo alfajiri lakini uongozi wa Yanga umelalamika kutokana na mchezaji huyo kushindwa kuaga na kujiondokea pasipo ruhusa.
Msemaji wa Yanga Jerry Muro ameiambia Goal wamehuzunishwa na kitendo kilichofanywa na mchezaji huyo kwa sababu walikuwa wanajua taarifa zake za kwenda kufanya majaribio Afrika Kusini lakini walimtaka asubiri ligi imalizike ndiyo aweze kwenda.
“Tuna mechi ya Ligi ya Vodacom dhidi ya Azam leo lakini bado tunamchezo mmoja wa mwisho na Ndanda FC, Mei 9 mechi zote hizo tulikuwa tunamtegemea lakini ameondoka tutajua adhabu ya kumpa pindi atakaporudi,”amesema Muro.
Msuva anatarajia kuanza majaribio kesho baada ya kufika na kupumzika leo na majaribio hayo yatatumia wiki moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni