Baada ya tetesi za muda mrefu, hatimaye
mambo yameamilika baada ya Yanga kufanikiwa kumsajili kiungo Haruna Chanongo.
Yanga imemsajili Chanongo akitokea Simba
ambayo ilikuwa imepeleka Stand United kwa mkopo.
Suala la usajili wa Chanongo limekamilika
jana kwa mkataba wa miaka miwili na sasa ni mchezaji halali wa Yanga.
Chanongo alipelekwa Stand United United huku
viongozi wa Simba wakiwa wanamshutumu kwa kitendo chake cha dharau.
Walisema alikuwa akiihujumu timu yao, jambo ambalo lilikanushwa na meneja wake Jamal Kisongo.
Simba walidai hata baada ya kuitwa na
viongozi wa juu akiwemo Rais wao, Evans Aveva, Chanongo alionyesha dharau.
Hali iliyowafanya waamini alikuwa akifanya hivyo kwa makusudi kwa kuwa ana “damu” ya Yanga.
CHANZO; SALEH JEMBE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni