STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 11 Mei 2015

Yanga yazuia wachezaji wake kujiunga Taifa Stars


Wahcezaji wa timu ya Yanga wamezuiliwa na uongozi wa timu hiyo kujiunga na tumu ya taifa 'Taifa Stars' wakitakiwa wapumzike
Wachezaji wa timu ya Yanga wamezuiliwa na uongozi wa timu hiyo kujiunga na tumu ya taifa ‘Taifa Stars’ wakitakiwa wapumzike
Wakati kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kikiingia kambini jana jioni kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya COSAFA itakayopigwa nchini Afrika Kusini, uongozi wa mabingwa wapya wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga umewazuia wachezaji wake kujiunga na kikosi hicho kwa madai kwamba wanahitaji mapumziko baada ya patashika za ligi kuu na michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Katibu mkuu wa Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amesema, uamuzi huo umechukuliwa kwa kuzingatia michuano ya COSAFA haipo kwenye orodha ya mashindano ya CAF.
“Ukweli upo, tumewaomba wenzetu wa TFF wawaangalie wachezaji wetu kwasababu hatatulipokuwa Tunisia kuna baadhi ya wachezaji waliomba wapumzike kwasababu walikuwa wanajisikia wamechoka na hawa wachezaji kwa mtu anyejua mwenendo wa sayansi ya michezo au mwili wa binadamu uanelewa mchezaji anapofikia kipindi anaomba apumzishwe anakuwa hapendi hata kufanya mazoezi ya mara kwa mara”, amesema Tiboroha.
“Sisi tumetoa angalizo kwa wenzetu ikiwezekana wawaruhusu hawa wachezaji wetu ili wapumzike anagalau hata kwa wiki tatu na baadae waendelee na ratiba ya mbeleni ambayo ipo, wachezaji hao watatumiwa kwenye michezo mingine ya kufuzu kucheza AFCON pamoja na CHAN”, alifafanua Tiboroha.
Katibu mkuuwa wa TFF Selestine Mwesigwa alipoulizwa juu ya madai hayo ya Yanga kutaka wachezaji wake wapumzishwe alisema hoja hiyo kimsingi haina mashiko.
“Sijapokea taarifa ya kambi kwa maana kujua wachezaji wangapi wameripoti lakini nategemea kuipata ili nijue wachezaji wangapi na kutoka timu zipi tayari wamesharipoti kambini na wangapi ambao bado hawajaripo na kwasababu gani bado hawajafika”, amesema Mwesigwa.
“Mashindano ya COSAFA yapo kwenye kalenda ya FIFA watu waingie kwenye tovuti ya FIFA watayaona mashindano hayo na mechi zote zinazoihusu Tanzania zilizopo kwenye kalenda hiyo zikiwemo hizi ambazo zitaanza kuchezwa siku za hivi karibuni huko Afrika ya Kusini”, ameongeza Mwesigwa.
“Kwahiyo si kweli kwamba haya mashindano hayapo kwenye kalenda ya FIFA, timu yetu ina watu wenye ueledi kwenye masuala ya soka, kuna madaktari na wataalamu wa mazoezi wao wanajua ni mazoezi ya aina gani yanafaa kwa mtu aliyechoka au aliyecheza mechi 40. Lakini Tanzania hakuna mchezaji anaefikisha mechi 40 na wala si timu moja inayocheza ligi, kwa hiyo hoja ya Yanga haina mashiko”, Mwesigwa alimaliza.
Lakini huko kwenye kambi ya Taifa Stars, kocha msaidizi wa timu hiyo Salum Mayanga amesema wachezaji tayari wameanza kuwasili kambini.
“Wachezaji tayari wameanza kuripoti kambini japo sijajua bado idadi kamili lakini kila mchezaji ambaye anawasili anatakiwa kumuona daktari ili afanyiwe vipimo kwanza”, amesema Mayanga.
“Sisi hatuna taarifa kwamba wachezaji wa Yanga wamezuiliwa, tunajua wataripoti kambini na baadhi yao tayari wapo kambini sio wote walioripoti lakini tunatarajia wote walioitwa wataripoti”, Mayanga amefafanua.
Juma lililopita kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij alitangaza kikosi cha wachezaji 28 kitakachoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya COSAFA itakayopigwa nchini Afrika Kusini ambako Tanzania itashiiki kama mgeni mualikwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox