Mshambuliaji wa Simba SC Danny Sserunkuma ameandika ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter unaoashiria kwamba maisha yake ndani ya klabu hiyo yamefikia ukingoni na sasa atakwenda kutafuta maisha sehemu nyingine ili kuendeleza soka lake.
Sserunkuma ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uganda, alijiunga na ‘Wekundu wa Msimbazi’ msimu uliomalizika juma lililopita akitokea klabu ya Gor Mahia FC ya Kenya ambako aliibuka mfungaji bora kwenye ligi ya Kenya (Kenyan Premier League) kabla ya kutua Simba.
Toka ametua Simba ameshindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza huku kocha mpya Goran Kopunovic aliyechukua nafasi ya Patrick Phiri amekuwa akiwatumia Ibrahim Ajib, Simon Sserunkuma na Elius Maguri kwenye nafasi ya ushambuliaji hali iliyomfanya Sserunkuma kukosa kabisa nafasi kwenye kikosi hicho.
Kuna wakati iliripotiwa kuwa mchezaji huyo hana uwezo wa kuona mbali lakini mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Zacharia Hans Poppe alikanusha taarifa hizo na kusema hajapata taarifa hizo lakini akasema, daktari wa timu ndio mwenye uwezo wa kuzungumzia taarifa hizo.mba ambao wametoa taarifa kwenye page zao za social mediak kwamba hawatakuwa tena na Simba msimu ujao.
Kwa upande wa Owino yeye mkataba wake umemalizika na hajataka kuongeza mwingine
Angalia walivyoandika kwenye kurasa zao za Twitter
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni