Wiki iliyopita PSV na United zilikubaliana dili la euro milioni 27.5 kwa ajili ya usajili wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye ataungana na Van Gaal baada ya kukamilisha vipimo vya afya majira ya kiangazi.
Mkurugenzi wa michezo wa PSV, Marcel Brands amedai mabingwa hao wa Uholanzi tayari walikuwa wamepanga kuanza mazungumzo na PSG kabla ya United hawajawapiga bao na Depay anakiri Van Gaal ndio chanzo kikubwa cha yeye kuamua kwenda Ligi Kuu.
Depay amesema alikaribia kwenda PSG kwani alikuwa akijua United walikuwa wakimtaka lakini hakuwaona kuwa makini mpaka dakika za mwisho wakati Van Gaal alipompigia simu na kuzungumza nae.
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa alikuwa na wakati mgumu lakini baada ya kuzungumza na Van Gaal akaamua kujiunga na United.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni