Kiungo
kutoka nchini Ubelgiji, Marouane Fellaini ameupinga ujumbe ulioandikwa
katika akaunti yake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, kumuhusu
mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Argentina Angel di Maria.
Kiungo
huyo wa klabu ya Man Utd, ameshutumiwa kuandika ujumbe wa kumtakia kila
la kheri Di Maria katika maisha yake mapya atakapokua na klabu bingwa
nchini Ufaransa Paris St Germain *PSG* msimu ujao wa ligi, kwa kuamini
ni mchezaji mwenye hadhi kubwa duniani.
Kituo
cha televisheni cha nchini Ufaransa *Telefoot* kiliuonyesha ujumbe
unaodaiwa kuandikwa na Fellaini kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter
ambao ulisomeka “Angel di Maria atakuwa chaguo sahihi kwa mabingwa wa
nchini Ufaransa PSG endapo atasajiliwa na klabu hiyo:
Fellaini
amesema hakuandika ujumbe huo katika mtandao wa Twitter na anahisi
mbinu zinazofanywa kwa sasa ni kutaka kumgombanisha na baadhi ya
viongozi huko Old Trafford ambao watakua wamekasirishwa na ripoti hiyo
iliyotolewa na kituo cha televisheni cha nchini Ufaransa.
Pia
kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, amedai kutengezenewa mazingira
mabaya dhidi ya mchezaji mwenzake Angel di Maria, ambapo anaamini atakua
hakupendezwa na taarifa hiyo.
Angel
di Maria amekua katika minong’ono ya muda mrefu ya kuwa mbioni kuondoka
Old Trafford, baada ya kushindwa kuonyesha uwezo wake tangu
aliposajiliwa na Man Utd mwanzoni mwa msimu wa 2014-15.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni