STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 8 Juni 2015

MAFUGO KUTUA MSIMBAZI MUDA WOWOTE




                                                   MAFUGO KUTUA MSIMBAZI MUDA WOWOTE

SIMBA imeamua kufanya mambo yake kimyakimya na kufanikiwa kunasa mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo.
Habari za uhakika zimeeleza, Simba imemsajili Mavugo kwa mkataba wa miaka miwili na mjumbe wa kamati ya utendaji, Collins Frisch ndiye alifanya kazi hiyo mjini Bujumbura, wiki iliyopita.
 
“Kweli alikuja hapa yule ofisa wa Simba, wamemalizana na Mavugo na kila kitu kimekwenda sawa,” Chanzo kutoka Bujumbura kimekaririwa
Hata hivyo imekuwa ikielezwa kwamba Mavugo ana mkataba binafsi na bosi wa timu yake ya Vital'O jambo ambalo Simba lazima walimalize kabla ya kupata uhamisho.
 
Simba ilikuwa ikishindwa kufanikisha dili hilo kwa straika huyo aliyekuwa akikipiga katika timu ya Vital’O baada ya kuibuka kwa machafuko ya kisiasa yaliyoenea nchini Burundi kutokana na baadhi ya raia wa nchi hiyo kupinga kitendo cha Rais Pierre Nkurunziza kuwania nafasi hiyo kwa awamu ya nne.
 
Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Simba, Collin Frisch alitinga Burundi kwa ajili ya kwenda kujua mbivu na mbichi juu ya hatma ya kumtia mikononi mchezaji huyo na hatimaye akarejea na jibu zuri.

Mavugo aliyewahi kuzitumikia Polisi ya Rwanda na SC Kiyovu anatua Simba akiondoka na rekodi nzuri nchini Burundi baada ya kuisaidia kwa kiasi kikubwa kutwaa ubingwa wa ligi ya Burundi msimu wa 2014/15.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox