STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 6 Juni 2015

MWISHO YA MAJADILIANO KATI YA CHOI NA MALDIN, KUELEKEA FAINALI YA LEO

     Yamesemwa mengi sana ila mwisho wa siku leo ndo leo asemae kesho ni muongo kila pande imejigamba wana wa Blaugrana vilevile Vecchia Signora  wa Turin mimi yangu macho si hitaji kujiita mkwezi mbele ya kambi ya wakwezi ukweli wa mambo ni Olympiastadion kwenye msimu wa 60 wa mashindano ya vilabu barani Ulaya na msimu wa 23 tangu muangazo mpya wa mashindano haya.


 Mwamuzi wa mchezo huo ni CUNETY CAKIR atakaesimama  katika dimba la Olympia stadion   ndani ya Jiji  Berlin ana umri wa miaka 38 akiwa amezaliwa huko Instabul,Uturuki 23/11/1976 , amechezesha zaidi ya michezo 170 huku mchezo wake wa kwanza  wa uefa champions league  ulikuwa kati ya Skonto fc vs Sliema wanderers julai 2003  kama kamisaa Aidha  sept 29 2010 alichezasha mcheza wa Cl hatua ya makundi kati ya Rubin Kazan na FC  Barcelona mchezo huo uliisha kwa timu zote kutokufungana , pia alichezesha mchezo kati ya Chelesea na Spartak Moscow.


       Raia huyu wa Uturuki pia atakumbukwa kwa kumpiga kadi nyekundu John Terry katika kipindi cha kwanza  kwenye nusu fainal ya uefa kati ya Chelsea  na Barcelona mchezo ulioisha  kwa sare ya 2-2 na kushuhudia Chelsea akitinga fainal na kubeba kombe hilo chini ya Roberto Di Mateo, bila kusahau mchezo wa Manchester utd dhidi ya Real madrid ambapo atakumbukwa na mashabiki wa United kwa kitendo cha kumpa Luis Nani kadi nyekundu kumbuka game hiyo ndo ilikuwa ya mwisho kwa Mzee Ferguson kwenye Uefa.


      kwa maana hiyo michezo yote ya fc barcelona aliyo chezesha timu hiyo ilitoka sare ingawa leo haito lala kitanukishwa mpaka kieleweke
  
                                                  MALDIN

FC BARCELONA;

      Walikuwa vinara katika group F' kwa jumla ya pointi 15 ,kwenye hatua ya 16 bora walikipiga dhidi ya Manchester City na waliibuka na ushindi wa jumla goli 3-1, robo fainal wakacheza dhidi  Paris Saint-Germain napo hawakufanya makosa kwa kuwachambanga mabingwa hao wa Ufaransa  kwa jumla ya goli 5-1, upande wa nusu fainal walipambana na 'The Bavarian'  chini ya kocha wao wa zamani Pep Guardiola mwisho wa siku walifanikiwa kuwachapa goli 5-3 ushindi wa jumla na baada ya hapo wakafudhu hatua ya fainal .
  
     Mpaka sasa Blaugrana wamefunga jumla ya magoli 28 kinara wa magoli ni Lionel Messi mwenye magoli 10 ndani ya dakika 1057 alizocheza, Neymar anamagoli 9 kwenye dakika 936 alizo kipiga, Luis Suarez kapachika magoli 6 katika dakika 737 alizo cheza kwa maana hiyo safu ya ushambuliaji ya Barcelona MSN-KOMBINENGA,KOMBINESHENI DE AMERICA  ina jumla ya magoli 25.
  
JUVENTUS;
  
       Kibibi kizee walikuwa group A' kama washindi wa pili kwa pointi 10 ,hatua ya 16 bora walikwaana na Borussia Dortmund na kuibuka na ushindi wa jumla 5-1 ,kisha waka kwea hadi robo fainal wakakipiga dhidi ya Monaco ya kule nchini Ufaransa na mwisho wa siku wakaibuka na ushindi wa jumla goli 1-0 walilo lifunga pale Turin, baada ya hapo  wakajivinjari mpaka hatua ya nusu fainal wakakumbana na mabingwa watetezi Real Madrid mechi ambayo asilimia kubwa ya wapenda soka waka anza vuta taswira ya Real kupata mteremko kuelekea fainal na huenda wangetetea ubingwa wao ila mwisho wa siku umzaniae kumbe ndie sie mbwembwe za soka huwa dimbani kibibi kizee kikaibuka na ushindi wa jumla magoli 3-2 baada ya hapo tunawashuhudia kwenye fainal ya msimu huu.


         Vecchia Signora wao upande wao wana jumla ya magoli 16 kinara wao wa magoli ni Carlos Tevez mwenye magoli 7  ndani ya dakika 1066 alizo cheza anaemfuata ni Alvaro Morata anmagoli 4 kwenye dakika 659 alizo kipiga  na Artulo Vidal mwenye goli 1 katika dakika 966 kwa mantiki hiyo  MTV  UTATU WA TURINI unajumla ya magoli 12 pekee.
  

KUMBUKA
              *   Vilabu vya Uhispania na Italia vimekutana mara 44 tumeshuhudia sare 11, Hispania wakishinda mara 18 , Italia waki ibuka na ushindi marav 15.


              * Barcelona wamekutana mara 8 na Juventus kwenye michuano ya barani ulaya , Juventus wameshinda mmichezo 4, Barcelona wakaibuka na ushindi katika michezo 2 na kushuhudia sare 2 mara zote walizo kutana Juventus walifunga jumla ya magoli 10 kati ya 9 ya Barcelona.


             * Juventus wamepoteza fainali 3 zilizo pita mara ya mwisho kushinda ni fainali ya msimu wa 1995/96 mbele ya Ajax wakati wapinzani wao Barcelona wameshinda fainal zao 3 zilizo pita mara ya mwisho kupoteza ni fainali ya msimu wa 1993/94  dhidi ya Ac Milan.


          * Ni fainali ya 7 kwa timu za Hispania na Italia kukumbana  na fainali zilizo pita timu za Italia zimeshinda mara mbili dhidi ya timu za Uhispania .


     *Endapo Barcelona watwaa ubingwa huu utakuwa wa 5 na hivyo kuwa timu pekee iliyo twaa ubingwa huu mara nyingi zaidi tangu msimu mpya wa uefa uanze 1992.


             *Patrice Evra atakuwa mchezaji wa pili kucheza fainali tatu za mashindano haya kwenye timu 3 tofauti  (Monaco, Manchester United na Juventus), atakuwa sawa na injini ya kiholanzi  Clarence Seedorf aliecheza fainali akiwa na ( Milan, Ajax na Real Madrid).


         *  Timu zote zimetwaa vikombe viwili kwenye ligi zao za ndani Juventus wakichukua ubingwa wa ligi kuu nchini Italia Seria A pamoja na Coppa Italia wapinzani wao Barcelona wamechukua ubingwa wa kombe la mfalme na ligi kuu almarufu kama La-liga. hivyo kila upande unatafuta trebo kwa udi na uvumba .

MR'CHOI -KONA KALI- Kwa kuangazia pande zote kila timu ina ubora wake tuna wazungumzia Juventus ikiwa timu yenye viungo bora kabisa ambao wanasaidiana vyema na safu ya ulinzi katika upande wa kujihami bila kusahau mashambulizi yao ya kustukiza kwa kutumia vyema kasi ya Tevez kwa kumpitishia mipira hatarishi , Allegri kaunda kikosi kinacho jua kupambana katika engo zote  hawa ndo roho yake Claudio Marchisio ,Paul Pogba,Andrea Pirlo na  Arturo Vidal sasa ukijaribu kuangaza ni viungo bora mbele ya viungo wa Barca wabishi kwenye kila kona ama unaweza sema hawarembi.


  Kuelekea kwenye mchezo wa leo shughuli pevu itakuwa kwa  Claudio Marchisio na Paul Pogba kudili na Jordi Alba pamoja na  Daniel Alves  watu ambao pande zao ndo huwa kuna madhara kwa mantiki ya mipira mingi ya Barcelona  pasi huchezwa pembeni asilimia  27.6  upande wa kulia na upande wa kushoto asilimia  ni 26.8.

         Iko wazi hawataweza shindana kumiliki mpira na Barca kwa maana hiyo uwepesi wa mashambulizi ya kustukiza, mpira wa kasi ndo silaha kubwa moja ya madhaifu ya Barcelona ni mipira ya juu kitu ambacho kinaweza wapa faida pindi wakipa kona na kutupia krosi .
   Uwepo wa Andrea Barzagli kwa maana ya kutokuwepo kwa  Giorgio Chiellini haina maana safu ya ulinzi ya Juventus na cha kufanya ni kuziba njia kwenye zone yao pindi wakishambulia kwa maana Barcelona ni hatari sana kutokana na mpaka sasa magoli yao 28 takribani magoli 25 wamefunga ndani ya box bila kusahau faulo zisizo na mantiki.


         Barcelona wao liko wazi Neymar amekuwa akipoteza nafasi nyingi sana kwa uzembe amekuwa na utoto mwingi kitu ambacho anatakiwa akiepuke siku ya leo zaidi ya hapo kwa pale mbele wako vyema tatizo kubwa licha ya msimu huu kuimalika kwenye safu ya ulinzi ila bado wamekuwa si wazuri katika mipira ya juu hasa upande wa kumaki watu zaidi ya hapo ni kwa wao kuto lememaa sana pindi wakiwa na umiliki wa mpira kwa mantiki ya kutokuweka nafasi ya kushambuliwa kwa kustukizwa pindi wakipoteza mpira.


     UBASHIRI-Kwa kuangazia pande zote na dizaini ya mchezo utakavyo kuwa kwa maana ya upande mmoja kumiliki zaidi na mwingine kumiliki kwa maana ya mashambulizi ya kustukiza nawapa nafasi Barcelona kuibuka na ushindi wa goli 2-1 magoli ya pande zote yatafungwa na wachezaji wa bara la Amerika.
     

                                                     MALDIN


 JE NI MESSI,SUAREZ,NEYMAR NIKIMAANISHA MSN KOMBINENGA DE AMERICA AU NI MTV YAANI MORATA,TEVEZ,VIDAL   tuta waaga kesho maana bado kuna jambo



KWA MAONI;


      choikangta.ckt@gmail.com 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox