Mwesigwa
SEKRETARIETI ya Shirikisho la soka Tanzania TFF imeamua
kuachana na sakata la utata wa mkataba wa Ramadhan Singano ‘Messi’ na klabu yake
ya Simba ikitaka upande ambao
haujaridhika na maamuzi uende kwenye vyombo vya juu zaidi.
Katibu mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa amekaririwa usiku huu
akisema wao kama wasuluhishi walishatoa ushauri wao na kwasasa hawataki
kuingilia kati.
“Sisi tuna diplomasia zinazosema kwamba, unaposuluhisha mgogoro hatakiwa tena kuingilia
katikati, mimi kama msuluhishi, si vizuri kusema chochote kuhusu Simba au
Singano”. Amesema Mwesigwa.
Rais wa Simba, Evans Aveva leo ametoa tamko kwamba klabu hiyo
haiwezi kukaa na Singano kujadili mkataba mpya kama walivyoshauri TFF kwasababu
mkataba wa mchezaji unaisha Julai 2016,
lakini Mwesigwa amesema hajapokea taarifa yoyote kutoka Simba.
“Mimi sijasikia chochote kutoka kwa Simba, kama kuna
chochote kutoka kwao wataleta. Siku zote linapotokea tatizo, TFF tunaangalia
njia rahisi ya kutatua, kama halina utata mkubwa basi tunalimaliza bila
kuhusisha kamati nyingi. Mikataba tunayokuwa nayo inaletwa na klabu na kwenye
mfumo inaingizwa na klabu, mkataba tulionao lazima unafanana na ule wa Simba
waliotuletea”
“Mchezaji ana mkataba wenye tarehe tofauti na waliotuletea
Simba, ndio maana tukasema ina utata. Yeyote ambaye hajaridhika akazungumze
kwasababu kuna vikao vingi tu huko juu,
anaweza kuendelea”.
Kwa maana hiyo kama Singano na Simba wataendelea kuvutana,
itabidi suala lao lipelekwe kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji ili kujua
mkataba upi ni sahihi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni