Mario
Balotelli amewataka mashabiki wa Liverpool kumsapoti Raheem Sterling
baada ya kuondoka klabuni hapo kujiunga na Manchester City.
Sterling leo amecheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha Man City chini ya Manuel Pellegrini.
Katika
mechi hiyo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya, Sterling amefunga
goli katika sare ya 2-2 ndani ya dakika za kawaida, kabla ya Man City
kushinda kwa penalti 5-4.
Muda mfupi baada ya mechi, Super Mario ame-tweet kumpongeza Sterling kwa kuanza vizuri.
Mashabiki wengi wa Liverpool wanaona Sterling ni msaliti kwasababu ya kulazimisha kuondoka Anfield.
Soma Tweets za Mario hapo chini akiwajibu mashabiki wa Liverpool wenye hasira:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni