Imeripotiwa
kwamba Messi alikua anatimiza ahadi yake ya kutembelea Gabon kwa Rais
Ali Bongo ambae anashutuma nyingi za udicteta na kula rushwa.
Bila
kutegemea Messi akiwa na Deco walifika nchini Gabon na Messi kuweka jiwe
la msingi kwenye ujenzi wa uwanja wa Taifa wa Gabon.
Ripoti
zilizotoka kwa wana habari wa ufaransa zinasema kwamba Messi alipokea
kiasi cha £2.4m ikiwa kama malipo yake ya kutembelea nchi hiyo. Mwanzoni
ziara hiyo ilipewa picha kama ni ya kujitolea kwenda kuzindua uwanja wa
taifa wa nchi hiyo.
Wachambuzi
wa mambo wanasema kwamba kwa status ya Messi hata kama angepewa mualiko
na Rais huyo ingekua sio rahisi kwa yeye kukubali kwasababu Rais huyo
ana sifa mbaya ya kula rushwa. Pia ana kashfa ya kujilimbikizia mali
wakati wananchi wake wana hali mbaya na nchi yake ina watoto wengi
wanaoishi kwenye umaskini.
Wapinzani
wa kisiasa wa Ali Bongo wanasema kwamba Rais huyo ametumia pesa za
walipa kodi kumlipa Messi ambaye anajihusisha sana na mambo ya kujitolea
duniani. Pia Ali Bongo inasemekana amemtumia Messi kwa ajili ya
kujipatia ushawishi zaidi kwa wananchi wake.
Pia
Messi aliweka mikono yake kwenye cement mbichi ambapo mikono yake
itabaki kama kumbukumbu uwanjani hapo.Messi na Baba yake bado wana kesi
ya ukwepaji wa kodi nchini Hispania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni