Mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi anatarajiwa kuondoka kwenda nchini Denmark katika klabu ya Sonderjyske iliyopo kwenye Danish Superliga. Majaribio hayo yatakuwa ya siku 14 kuanzia tarehe 08/07/2015 na baada ya hapo klabu hiyo ya Sonderjyske itatuma ripoti kamili ya majaribio yake.
Rais wa Simba Evans Aveva alisema “Simba inafurahi sana kuona wachezaji wake wanapata nafasi hizi za kuonesha vipaji vyao tena kwenye viwango vya kimataifa zaidi, hivyo Simba inamtakia kila la kheri Okwi kwenye majaribio yake ya siku 14 kwnye klabu ya Sonderjyske iliyopo kwenye Danish Superliga”.
Okwi alizaliwa Desemba 25, 1992 Kampala Uganda anachezea timu ya Taifa ya Uganda kama mshambuliaji wenye jezi namba 10.
Simbasports.co.tz inamtakia kila la kheri Emmanuel Okwi, tutaendelea kuwaletea maendeleo ya majaribio yake kadiri tutakavyopata.
Wakati huo huo mchezaji Jonas Mkude aliyekuwa nchini Afrika ya Kusini kwa majaribio kwenye klabu ya Bidvest Wits, amerejea nchini baada ya kumaliza muda wa majaribio yake. Kwa mujibu wa taarifa toka katika klabu ya Bidvest, Jonas ameonyesha kiwango kizuri, hivyo wanafanya mipango ya kumpa nafasi nyingine hapo baadae kwenda nchini Afrika ya Kusini huku wakimfuatilia kwa karibu zaidi akiwa na klabu yake ya Simba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni