SHIRIKISHO la Soka la Nigeria-NFF limetengua mkataba wa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Stephen Keshi baada ya Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo kukutana katika kikao cha dharura jijini Abuja.
Katika taarifa yake shirikisho limedai kufuatia taarifa zilizowasilishwa na kamati ya nidhamu, ufundi na maendeleo wameamua kusitisha ajira ya Keshi kutokana na mambo kadhaa kubwa ikiwa ni kutokuwa na moyo wa dhati wa kufanya kazi hiyo.
Keshi amekuwa chini ya shinikizo toka taarifa zivuje kuwa aliomba kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Ivory Coast na hilo ndio linahisiwa kuwa jambo kubwa lililomfukuzisha kazi. Kikosi cha nchi hiyo maarufu kama Super Eagles sasa kitaongozwa na aliyekuwa kocha msaidizi Salisu Yusuf kwa muda huku kamati ya ufundi ikiongozwa na Shuaibu Amodu mpaka hapo atakapopatikana kocha mpya. Keshi mwenye umri wa miaka 53, alianza kuinoa Super Eagles mwaka 2011 huku akifanikiwa kushinda taji la Mataifa ya Afrika mwaka 2013.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni