Klabu ya PSG imejitosa kupambana na klabu ya soka ya Real Madrid kuwania saini ya mchezaji Eden Hazard wa Chelsea katika majira ya kiangazi mwakani.
Hazard raia wa Ubelgiji amekua akihusishwa hivi karibuni kuhamia katika klabu ya Real Madrid na sasa PSG imeingia katika mchakato huo.
Inaelezwa kuwa pamoja na Hazard kuongeza mkataba wa miaka 5 msimu uliopita klabuni hapo, hana furaha na kwamba akili yake iko Real Madrid huku pia kukiwa na tetesi huenda hawana uhusiano mzuri na kocha Jose Mourinho ambaye amekua akiwaongelea wachezaji wake tofauti na awali.
Klabu ya PSG ya Ufaransa inaamini Hazard ambaye alishawahi ichezea klabu ya Lille ya nchini Ufaransa, atakua radhi kurudi tena nchini humo.
Inaelezwa mkataba wa Hazard na Chelsea unafanya thamani ya mchezaji huyo kuwa inakaribia pauni milioni 80 na kwamba PSG wako tayari kumtwaa mchezaji huyo bora wa msimu uliopita katika ligi ya England.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni