TIKETI za mchezo wa
kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia chini Urusi mwaka 2018 kati
ya Tanzania dhidi ya Algeria zitaanza kuuzwa kesho Ijumaa katika vituo
10 viliyopo jijini Dar es salaam.
Magari maalumu yenye stika yataanza
kuuza tiketi hizo za mchezo kesho saa 2 kamili asubuhi mpaka saa 12
jioni, ambapo tiketi zinauzwa kwa shilingi elfu tano (5,000) kwa viti
vya rangi ya bluu na kijani na rangi ya machungwa, na elfu kumi (10,000)
kwa viti vya VIP B & C.
Vituo vitakavyotumika kuuza tiketi hizo ni
ofisi za TFF – Karume, Buguruni – Oilcom, Mbagala – Darlive, Mnazi
Mmoja, Luther House – Posta, Big Bone – Msimbazi, Ubungo – Oilcom,
Makumbusho – Stand ya Daladala, Uwanja wa Uhuru.
TFF inawaomba wadau,
washabiki na watanzania kujitokeza kwa wingi kununua tiketi za mchezo
huo katika magari maalumu yatakayokuwepo kwenye vituo vilivyotajwa, ili
kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizokuwa halali.
Wakati huo huo
Ubalozi wa Algeria nchini Tanzania, umewataka waandishi wa habari
wanaotrajia kwenda kuripoti mchezo wa marudiano jijini Algiers siku ya
jumanne, kuwasilisha maelezo ya chombo wanachofanyia kazi pamoja na
vifaa watakavyovitumia kwenye mchezo huo (camera, vinasa sauti)
kuwasilisha maelezo hayo leo Alhamsi kabla ya saa 9 mchana katika ofisi
za Ubalozi huo kwa ajili ya kupatiwa Accreditation za kufanyia
kazi.
Matokeo ya mchezo wa jana Azam Sports Federtaion Cup (ASFC), ni
Mshikamano 0 - 1 Cosmopolitan,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni