RAIS wa Shirikisho la
Soka la Duniani-FIFA, Sepp Blatter amelazwa hospitalini kutokana na
kupatwa mshituko wa neva.
Blatter aliyesimamishwa kwa siku 90
kujishughulisha na masuala ya soka wakati akichunguzwa kwa kashfa za
rushwa , alilazwa hospitalini kwa ajili ya uchunguzi wa afya lakini sasa
imeelezwa ataendelea kubaki huko.
Blatter aliyeongoza shirikisho hilo
kwa miaka 18 mpaka sasa, awali ilidaiwa alikuwa na matatizo ya msongo wa
mawazo hivyo ikabidi apate huduma ya matabibu, sasa imebainika ana
tatizo la mshituko wa neva.
Awali, mwanasheria wake, Richard Cullen
alieleza juu ya uangalizi huo wa madaktari kutarajiwa, lakini akasema
alitarajia arejee nyumbani mapema kabla hali kubadilika na kutolewa
maelezo tofauti.
Hata hivyo, watu wake wa karibu wameeleza hali yake si
mbaya na anatarajiwa kurejea katika hali ya kawaida japokuwa atabaki
hospitalini hadi mapema wiki ijayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni