SHIRIKISHO la Soka
Duniani-FIFA limelichuja jina la rais wa Shirikisho la Soka la Liberia,
Musa Bility katika kinyang’anyiro cha urais wa shirikishi hilo.
FIFA
limepitisha majina ya wagombea watano wa nafasi hiyo huku jina la rais
wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA Michel Platini aliyesimamishwa
likiwa halijajumuishwa.
Platini raia wa Ufaransa jina lake linaweza
kuongezwa katika orodha hiyo kama adhabu yake ya kusimamishwa itakwisha
kabla ya Februari ambapo uchaguzi utafanyika.
Majina matano
yaliyopitishwa ni pamoja na Prince Ali bin al-Hussein, Jerome Champagne,
Gianni Infantino, Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa na Tokyo
Sexwale.
Katika maelezo yake FIFA haikufafanua kwanini haswa walimkata
Bility lakini anaweza kukata rufani kupinga uamuzi huo katika Mahakama
ya Kimataifa ya Michezo-CAS.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni