Kuelekea michuano ya mataifa ya Ulaya
yatakayofanyika mwaka 2016, shirikisho la soka barani Ulaya limetangaza
mpira maalum kwa ajili ya kutumika katika mashindano hayo, mpira wa
utaotumika katika mashindano hayo ya mataifa ya Ulaya kwa mwaka 2016
umetengenezwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya kijerumani ADIDAS.
Mpira huo maalum wa Euro unaoitwa kwa jina la kifaransa la ‘Beau Jeu’ ambapo kwa kiingereza unatafsiriwa kwa jina la ‘the beautiful game’ unatajwa kufanana na mpira (Brazuca) uliotumika katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 iliyofanyika Brazil . Mpira wa ‘Beau Jeu’ ulitengenezwa kwa zaidi ya miezi 18.
Michuano ya Euro 2016 itafafanyika Ufaransa lakini ADIDAS imekuwa ikipokea tenda ya kutengeneza mipira ya mashindano hayo kwa miaka mingi sasa.
Hii ni List ya mipira ya Euro iliyokuwa inatumika kuanzia mwaka 1960 hadi utakaotumika mwaka 2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni