Mchezaji mwenye umri wa miaka 48 ametia saini mkataba wa kuendelea kuchezea klabu ya Yokohama FC nchini Japan.
Kazuyoshi alianza kuchezea klabu ya Santos akiwa na umri wa miaka 15 mwaka 1986, na mkataba huo wake utafikisha kipindi alichocheza soka kuwa miaka 30.
"Nashukuru sana maafisa wa klabu na mashabiki ambao wamekuwa wakiniunga mkono,” alisema Kazuyoshi, ambaye amefungia timu ya taifa ya Japan mabao 55 katika mechi 89.
"Nitaendelea kujitolea katika uchezaji wangu,” alisema.
Kazu amewahi kuchezea klabu za Genoa na Dinamo Zagreb barani Ulaya na ndiye anayeshikilia rekodi ya kuwa mchezaji mkongwe zaidi kufunga bao mechi ya ushindani Japan. Alifunga bao hilo mechi ya ligi ya daraja la pili miezi minne baada ya kutimiza umri wa miaka 48.
Alisaidia Japan kufuzu kwa Kombe la Dunia 1998, akiwafungia mabao 14. Alichezea timu ya taifa mara ya mwisho 2000.
Ni wachezaji wachache sana huendelea kucheza wakiwa na umri mkubwa hivyo, .
Wiki iliyopita kwa mfano, mshambuliaji wa zamani wa Uingereza Teddy Sheringham alijiandikisha kama mchezaji wa klabu ya Stevenage, ambayo yeye ndiye meneja, akiwa na umri wa miaka 49.
Hata hivyo, hakucheza katika shindano la kombe la nyumbani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni