Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo
anaripotiwa kutumia mkwanja mrefu kununua ndege binafsi, Staa huyo
anayeongoza katika list ya rekodi ya watu maarufu wanaongoza kupata
likes nyingi katika mtandao wa facebook amenunua ndege binafsi aina ya Gulfstream G200 Business Jet.
Ronaldo mwenye
umri wa miaka 30 anatajwa kununua ndege hiyo kwa thamani ya pound
milioni 13.5 ambazo ni zaidi ya bilioni 44 za kibongo kwa ajili ya
kuzunguuka sehemu mbalimbali duniani kuhusiana na mipango yake ya
kujitanua kibiashara, ndege ya staa huyo inatajwa kuwa na uwezo wa
kubeba watu 8 hadi 10, jiko la umeme, bafu, friji, makabati, simu na
internet.
Staa huyo ambaye anaonekana kujiimarisha
zaidi kibiashara tayari amezindua movie ya maisha yake halisi
aliyoizindua hivi karibuni Uingereza ila mwaka 2015 alitajwa kuzindua perfume, brand ya viatu vyake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni